Opresheni ya kuachiliwa waasi yasambaratika | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 01.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Opresheni ya kuachiliwa waasi yasambaratika

---

BOGOTA

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amesema waasi wa Colombia wamekataa kuwaachia huru mateka watatu kwa kile walichokitaja kuwepo kwa opresheni za wanajeshi wa serikali kinyume na masharti waliyotoa.

Maafisa wa serikali ya Colombia hata hivyo wamekanusha kuwepo kwa opresheni zozote za kijeshi na wamewalaumu waasi kwa kushindwa kueleza ni wapi mateka hao wangechukuliwa baada ya kuachwa huru.Hata hivyo rais Chavez ambaye ni mpatanishi katika suala hilo la kuwashawishi waasi wawaachie huru mateka,amesema opresheni hiyo itaendelea.Mateka waliokuwa wamepangiwa kuachwa huru niClara Rojas,msaidizi wa aliyekuwa mgombea wa urais Ingrid Bentancourt ambao walitekwa nyara mwaka 2002 pamoja na mwanawe bi Rojas, Emanuel anayesemekana babake ni mmoja wa waasi na mateka mwingine ni mwanasiasa Consuelo Gonzalez De Perdomo aliyetekwa nyara mwaka 2001.

Ndege za kijeshi za Venezuela ambazo zilipaswa kuwachukua mateka hao tayari zinarudi nyumbani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com