1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uzalishaji wa mafuta kuendelea kuwa wa kiwango cha chini

Sudi Mnette
5 Desemba 2022

Mataifa yenye kuzalisha kwa wingi mafuta duniani yakubaliana kuendelea kupunguza kiwango cha mafuta wanachokizalisha ili kuendana na hali ya soko duniani.

https://p.dw.com/p/4KSxd
Organization of the Petroleum Exporting Countries (OPEC)
Picha: RYAD KRAMDI/AFP/Getty Images

Mataifa yenye nguvu kubwa katika uzalishaji wa mafuta duniani yanayoongozwa na Saudi Arabia na kwa upande mwingine Urusi yamehitimisha mkutano wao kwa kukubalina kudumisha viwango vyao vya sasa vya uzalishaji wa mafuta katika hali ya sintofahamu na ikiwa kabla ya kuanza kutekelezwa vikwazo vipya dhidi ya serikali ya Moscow vyenye kutarajiwa kuanza kuanza juma hili. 

Mataifa hayo 13 wanachama wa umoja wa OPEC wanaoongozwa na serikali ya Riyadh na washirika wao mataifa mengine 10 yenye kuongozwa na Urusi, kwa  ujumla wa mataifa 23 yakijulkana kama OPEC+ wameamua kuzingatia makubaliano ya Oktoba ya kupunguza uzalishaji wa mapipa milioni mbiili kwa siku hadi mwishoni mwa 2023.

Nafasi ya hatua za dharura zitakapohitajika

Lakini hata hivyo mataifa hayo, katika mkutano huo wamekubaliana kuchukua kukutana muda wowote kuanza sasa na kufanya mabadiliko yanayohitajika kwa kutegemea mahitaji ya soko.

Saudi Arabien | Öl-Lager am Hafen von Jubail
Eneo la uhifadhi wa mafuta Saudi ArabiaPicha: Bilal Qablan/AFP/Getty Images

Mchambuzi katika masuala ya nishati kutoka taasisi ijulikanayo kama ABN AMRO,Hans van Cleef  amesema uamuzi huo wa Jumapili ulitegemeewa sana  na kwamba hukuwa na la kushangaza,ikizingatiwa hali ya kudorora kwa uchumi, hatua ambayo imeshusha bei ya pipa la mafuta kufikia dola 90 pamoja na kupunguzwa huko kwa viwango vya uzaslishaji.

Muungano huo unaojulikanao kwa pamoja kama OPEC+, umesema uamuzi wake wa Oktoba wa kupunguza uzalishaji "ulisukumwa tu na hali juma la soko, na kuongeza kwamba umekuwa lazima kuwepo kwa njia ya lazima na sahiki katika kuleta hali tulivu katika soko kote duniani.

Punguzo la uzalishaji wa mafuta la Oktoba ni la kihistoria

Hatua ya upunguzaji wa uzalishaji mafuta ya  Oktoba kwa mataifa hayo yenye nguvu katika nishati hiyo inaakisi kiwango kikubwa zaidi cha punguzo  tangu kuongezeka kwa janga la Covid mwaka 2020, hatua iliyopingwa vikali la Marekani katika makabiliano yake na Urusi.

Mkutano unaofuata wa ngazi wa uwaziri kwa OPEC+ umepangwa kufanyika Juni 4, 2023. Lakini muungano huo ulisema uko tayari "kukutana wakati wowote na kuchukua hatua za ziada za haraka" kushughulikia mwenendo wa  soko na kusaidia soko la mafuta ikiwalazimu.

Ikumbukwe tu, Ijumaa iliyopita Umoja wa Ulaya na, na nchi tajiri yani G7 na Australia zilikubaliana kuweka ukomo wa bei ya mafuta kwa mafuta ya Urusi.  G7 na Australia zilikubaliana bei kikomo iwe dola 60 kwa pipa ambayo ilipendekezwa kutumia kuanzia Jumatatu hii au baadae kidogo baada ya kuanza kutekelezwa marufuku ya usafirishaji wa mafuta ghafi ya Urusi.

Soma zaidii:OPEC+ yaidhinisha hatua ya kupunguza uzalishaji wa mafuta

Marufuku hiyo itazuia usafirishaji wa mafuta ghafi ya Urusi kupitia bahari kuelekea ulaya ambayo yanakadiriwa kuwa theluthi mbili ya uagizaji wa umoja huko, jaribio ambalo linalengo la kuipunguzia serikali ya Urusi nguvu ya kifedha, katika kushiriki vita vya Ukraine kwa kukosa mabilioni ya Euro.

Chanzo: AFP