1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olmet akutana na Abbas

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Ch6W

JERUSALEM.Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais wa Mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas wanakutana kujaribu kutafuta muafaka katika suala ya ujenzi makaazi ya walowezi wa kiyahudi,suala linalotishia mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati.

Mkutano huo unaofanyika katika makaazi ya Waziri Mkuu huyo wa Israel ni wa kwanza kati viongozi hao wawili toka mkutano wa amani wa mwezi uliyopita huko Annapolis Marekani.

Viongozi hao walikubaliana kurejea tena katika mazungumzo ya amani ya Mashariki nya Kati yatakayopelekea kuundwa kwa taifa la Palestina, kabla ya kumalizika kwa kipindi cha Rais Bush mwakani.

Hata hivyo uamuzi wa serikali ya Israel kuendelea na ujenzi wa makaazi ya walowezi wa akiyahudi katika maeneo ya kaskazini mwa Jerusalem unaonekana kuzikwaza juhudi hizo.Palelstina wanadai eneo hilo ni huenda likawa makao makuu ya taifa lao.