1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Olimpiki: Fainali ya mbio za mita 100 Jumapili

Admin.WagnerD13 Agosti 2016

Siku ya nane ya michezo ya Olimpiki inahusisha heka heka za kuwania medali katika kuogelea, mbio na michezo mbali mbali ya uwanjani, kupigana na ufito wa chuma, fencing,mbio za baisikile na mengi mengine.

https://p.dw.com/p/1JhXv
Bildergalerie - Sport Highlights 2012
Usain Bolt kutoka JamaicaPicha: Getty Images

Hatimaye michezo hiyo itashuhudia nafasi adimu ya kumuona binadamu anayekimbia kwa kasi duniani. Usain Bolt , bingwa mtetezi mara mbili wa mbio za mita 100 anaingia uwanjani kwa mara ya kwanza katika mbio za mchujo mchana leo. Fainali zitafanyika kesho Jumapili, na Bolt amewaambia wazazi wake yuko tayari kwa fainali hizo licha ya kuwa ana maumivu kidogo katika paja.

Usain Bolt Rio 2016 Olympia 2016
Usain Bolt mkimbiaji wa mbio fupi kutoka JamaicaPicha: picture-alliance/dpa/Kappeler

Fainali ya wanawake ya mbio za mita 100 itafanyika leo Jumamosi ambapo watachuana Elaine Thomson wa Jamaica, Murielle Ahoure wa Cote d'Ivoire, Dafne Schippers wa Uholanzi na Wamarekani English Gardner, Tianna Bartolette na Tori Bowie.

Tirunesh Dibaba wa Ethiopia tayari amenyakua medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 mapema jana Ijumaa, sasa ni zamu ya mdogo wake Genzebe kuwania medali katika mbio za mita 1,500 leo. Genzebe bingwa wa dunia alifanikiwa kupita katika mbio za mchujo jana Ijumaa, na kuwaacha wapinzani wake kwa umbali mkubwa.

Olympia London 2012 Tirunesh Dibaba
Tirunesh Dibaba wa EthiopiaPicha: Reuters

Neymar na Colombia

Katika soka robo fainali zimekwisha anza siku moja baada ya Sweden kuifadhaisha marekani kwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti kwa upande wa soka ya wanawake.

Pambano linalosubiriwa kwa hamu ni kati ya Brazil na Colombia kwa upande wa wanaume, ambapo pambano hilo lina hisia zake kufuatia pambano la robo fainali la kombe la dunia mwaka 2014 ambapo Juan camillo Zuniga wa colombia alipiga kigoti mgongoni Neymar na kuvunja mfupa wa mgongo.

Rio 2016 Fussball Deutschland Südkorea
Wachezaji wa timu ya Ujerumani ya Olimpiki wakipambana na Korea kusiniPicha: Reuters/F. Donasci

Michezo mingine ni kati ya Ureno dhidi ya Ujerumani, Nigeria itaoneshana kazi na Denmark na Korea kusini dhidi a Honduras.

Kwa upande wa Tennis Mjerumani Angelique Kerber anawania dhahabu baada ya kuingia katika fainali dhidi ya Monica Puig wa Puerto Rico.

Super Cup

Kesho Jumapili nchini Ujerumani kutakuwa na pambano la kufungua msimu la kukata na shoka, ambapo mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanaikabili Borussia Dortmund iliyoshika anfasi ya pili katika ligi msimu uliopita katika Super Cup nchini Ujerumani.

Mats Hummels
Mats Hummels aliyekuwa nahodha wa Dortmund ameahamia Bayern MunichPicha: Imago/T. Frey

Pambano hilo linaiweka Ujerumani nzima katika hamasa kubwa, ukitilia maanani kuhama kwa wachezaji muhimu kutoka timu moja kwenda nyingine.

Mlinzi na nahodha wa zamani wa Borussia Dortmund Mats Hummels amehamia kwa mahasimu wao na alikoanzia soka Bayern Munich , wakati mchezaji wa kati Mario Goetze amerejea kundini kutoka Bayern Munich akielekea katika timu alikokulia Borussia Dortmund.

Mario Götze Fußball zurück zum BVB
Mario Goetze aliyekuwa Bayern Munich amehamia sasa Borussia DortmundPicha: picture-alliance/dpa/A.Gebert

Nako nchini Uhispania Barcelona wataingia dimbani kesho Jumapili kukabiliana na Sevilla katika pambano jingine la Super Cup nchini humo.

Deutschland DFB Pokal Finale FC Bayern München - Borussia Dortmund Pep Guardiola
Kocha wa Manchester City Pep GuardiolaPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Premier League Uingereza

Wakati huo huo Ligi ya Uingereza Premier League inarejea uwanjani leo ambapo mabingwa watetezi wanaumana na Hull City , Everton wanawakaribisha makamu bingwa Tottenham Hot Spurs, na Manchester City wako nyumbani wakiikaribisha Sundeland.

Kesho Jumapili patachimbika wakati Arsenal itaikabili Liverpool , Bournemouth iko nyumbani ikiisubirin Manchester United na Chelsea inatiana kifuani na West Ham United.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef