Obama | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Obama

Jana usiku ilikuwa ni siku ya kihistoria nchini Marekani na pengine kote duniani pale seneta Barack Obama alipohitimisha uteuzi wake wa kuwania urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya chama cha Demokratic

Seneta Barack Obama na mkewe Michelle Obama baada ya hotuba yake katika uwanja wa Invesco Field huko Denver mbele ya wafuasi wa chama chake cha Democratic jana

Seneta Barack Obama na mkewe Michelle Obama baada ya hotuba yake katika uwanja wa Invesco Field huko Denver mbele ya wafuasi wa chama chake cha Democratic jana


Hotuba ya Obama mbele ya umati wa wafuasi wa chama hicho wapatao elfu 75 katika uwanja wa mpira, ilikuwa ya kusisimua ambayo iliwatoa machozi wengi.


Barack Obama alikubali rasmi uteuzi wa kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu akichuana na mgombe wa chama cha Republican Seneta John MacCain


Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mgombea urais wa chama hicho kutoa hotuba ya kukubalia kuteuliwa nje ya ukumbi wa mkutano, toka mwaka 1960 wakati rais wa zamani marehemu John F Keneddy alipofanya hivyo .


Hotuba hiyo ya Obama hapo jana pia aliitoa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 45 toka kutolewa kwa hotuba maarufu ya mpigania haki za raia nchini humo ambaye alikuwa mwenye asili ya Afrika, Martin Luther King.Luther King katika hotuba hiyo alisema kuwa nina ndoto za kuona kuwa Marekani inakuwa moja isiyo na ubaguzi.


Obama alisema kuwa hotuba hiyo ya Marting Luther King miaka 45 iliyopita ilitoa mwanga wa majaaliwa ya Marekani moja.


John Lewis ambaye alikuwa miongoni mwa waandamanaji katika mkutano huo wa miaka 45 iliyopita alimuelezea Obama kama mtu atakayetimiza ndoto ya King.


Obama alisema kuwa huu ni wakati wa kuibadilisha Marekani kutoka katika siasa za Republican ambazo alisema zimeudidimiza uchumi wa nchi hiyo.


Hotuba yake iliwasisimua wengi na kuwatoa machozi, miongoni mwao akiwa mwaandaji maarufu wa vipindi vya majadiliano Oprah Winfrey ambaye aliondoka katika mkutano huo huku akisema kuwa hana kope kwania machozi yalikuwa mengi.


Akionekana kuteka mioyo ya watu lukuki wale waliyokuwa ndani ya uwanja huo na wale waliyokuwa wakifuatilia hotuba hiyo kwa njia ya rinunga, Obama alizidi kumwaga mafuta katika cheche za kuteka kura zaidi pale alipomsifu na kumshukuru aliyekuwa mpizani wake Hillary Clinton


Nchini Kenya Sarah Obama ambaye ni mke wa tatu wa babu yake Obama alisema kuwa ana imani kubwa kuwa mjukuu wake huyo ataweka historia ya kuwa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika nchini Marekani.


Bibi huyo amesema kuwa alijitahidi kuangalia hotuba hiyo ya mjukuu wake ambayo kwa saa za afrika mashariki ilikuwa usiku wa manane, lakini alishindwa kutokana na kutokuwepo umeme kijijini kwao.


Kwa upande mwengine Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambaye ni mjaluo kama alivyo baba yake Obama , alisema kuwa mafaniko ya Obama ni habari njema kwa Afrika.


Wanamuziki kadhaa maarufu kama vile Steve Wonder walitumbuiza saa tano kabla ya Obama kupanda jukwaani kutoa hotuba hiyo.

 • Tarehe 29.08.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F763
 • Tarehe 29.08.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F763
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com