1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama na ufumbuzi wake

29 Agosti 2008

Barack Obama amewaahidi wamarekani ufumbuzi wa matatizo yao.

https://p.dw.com/p/F74q
Obama na mkewe.Picha: AP

Hotuba ya Seneta Barack Obama,aliekubali jana rasmi kuwa mgombea wa wadhifa wa urais wa Marekani kwa chama cha Democratic Party,ikisubiriwa kwa hamu kubwa.Kwa hotuba hiyo mbele ya wajumbe wa chama na kwa wapigakura kote nchini,ulimalizika jana usiku mkutano mkuu wa chama cha Democrat.►

"Nimegundua suluhisho la matatizo yenu."-ndio risala alioitoa jana barack Obama mbele ya mkutano mkuu wa chama cha democrat.Na chama kikasimama wima nyuma yake.

Wademokrat walistahiki kweli parti ya jana.Walichukua miezi 8 kumsaka mtetezi wao wa wadhifa wa urais na mwishoe, kushikamana nae pamoja.

Katika vuguvugu la kampeni ya uchaguzi hasa kutoka kinywa cha Hillary Clinton na mumewe ,maneno machafu yalisikika dhidi ya Obama.Maneno ambayo katika mbio zake za kuingia Ikulu,mjini Washington ,yatamuandama na kumletea matatizo tena na tena .

Rasmi, chama cha Democratic party, kikikanusha kuwa kampeni ya uchaguzi wa mtetezi wa urais umekigawanya chama.Mshikamano uliobainishwa mkutanoni Denver,umedhihirisha dhahiri-shahiri kinyume chake.

Kwani, Denver imeonesha umoja na mshikamano wa chama.

Hillary Clinton,aliekua hasimu mkubwa wa Barack Obama katika kampeni hii ya uchaguzi,muda mfupi kabla, alihutubia na kusema, binadamu anabidi kubadilika ili kuwaleta pamoja wapigakura nyuma ya Obama.Na timu yake haikuregeza kamba katika kila juhidi za kuitimiza shabaha hiyo.Kwani, Hillary na mumewe Bill ,walipokewa mikono miwili na wakatumia nguvu zao zote za ushawishi wa kisiasa kuonesha umoja na seneta Obama.

Hawakufanya hivyo bila kutojali masilahi yao-kwani heba ya rais wa zamani Bill Clinton, iliathirika kutokana na hujuma zake alizolenga kwa seneta Obama.Akina Clinton, hawakumudu kumtilia Barack Obama kitumbua chake mchanga katika uchaguzi ujao wa rais Novemba hii.Kwahivyo, Hillary alishughulikia kutawazwa kitini na mapema kwa Obama kama mtetezi rtasmi wa chama.Na halafu mumewe Bill Clinton,alizungumza maneno ambayo hapo kabla, hakuyadhukuru:Alisema."Obama yutayari kuiongoza Marekani"- ni maneno ambayo wafuasi wote wa chama cha Democratic party, wakisubiri kusikia.Akakumbusha kwa mzaha: Hata yeye aliambiwa na warepublikan miaka 16 iliopita, kuwa" ni mchanga na hana maarifa."...

Jana usiku Barack Obama mwenye umri wa miaka 47, seneta wa Illinois, alibainisha wazi wazi jinsi alivyomsemaji mzuri mwenye nguvu za hoja na sio hoja za nguvu.Alibakia na staili yake ile ile,lakini hakuchelea pia kuhujumu.Alitambua kwamba, ikiwa ashinde uchaguzi wa Novemba wa kiti cha urais,lazima kuwaeleza wapigakura tena wazi wazi anapanga kuwatendea nini na sio porojo tu.Alieleza ni majibu gani anayo kwa matatizo yao......

Picha zilizotapakaa ulimwenguni kutoka Denver,zimeonesha ni za chama kilichoungana tena. Zimeonesha pia ni mtetezi wa Urais aliepania na kuvinjari kweli kupigania urais.