Obama haoni uwezekano wa kupeleka jeshi Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Obama haoni uwezekano wa kupeleka jeshi Syria

Rais wa marekani Barack Obama amekaribia siku ya Ijumaa(03.05.2013) kuamua kutowapeleka wanajeshi wa Marekani nchini Syria,akisema kuwa haoni uwezekano ambao hatua hiyo italeta manufaa kwa Marekani ama Syria.

US President Barack Obama waves as he steps off Air Force One upon arrival at Juan Santamaría International Airport on May 3, 2013 in San Jose, Costa Rica. Obama arrived in Costa Rica for a summit with Central American leaders focused on trade, immigration and the drug war following a 24-hour trip to Mexico. Obama's plane landed in San Jose around 1:50 pm (1950 GMT) amid heavy security in the capital, with many streets and shops closed ahead of his talks with the seven leaders of Central America, plus the Dominican Republic. AFP PHOTO/Mandel NGAN (Photo credit should read MANDEL NGAN/AFP/Getty Images)

Rais Barack Obama akiwasili mjini San Jose, Costa Rica

"Kama sheria ilivyo kwa jumla , siondoi uwezekano , kama mkuu wa majeshi kwasababu hali inabadilika na unataka kuhakikisha kuwa kila wakati nguvu za Marekani zinakuwapo kuweza kutimiza maslahi ya taifa ya kiusalama, " amesema Obama.

"Baada ya kusema hayo, siioni hali kwamba wanajeshi wa Marekani wataingia katika ardhi ya Syria , wanajeshi wa marekani nchini Syria , hawataleta manufaa kwa Marekani tu , lakini pia wataleta manufaa kwa Syria."

U.S. President Barack Obama laughs as comedian Conan O'Brien speaks during the White House Correspondents Association Dinner in Washington April 27, 2013. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS ENTERTAINMENT PROFILE TPX IMAGES OF THE DAY)

Rais Barack Obama

Uvumi umekuwa ukiongezeka kuwa utawala wa rais Obama unaweza kubadilisha upinzani wake wa kuwapa silaha waasi baada ya Ikulu ya nchi hiyo kusema wiki iliyopita kuwa rais Bashar al Assad huenda alitumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake.

Msitari mwekundu

Obama amekuwa akijizuwia kuingilia kati katika vita lakini anakabiliwa na ukosoaji kuwa ameruhusu utawala wa Assad kuvuka msitari mwekundu alioutangaza, iwapo zitatumika silaha za kemikali.

Rebel fighters from the Al-Ezz bin Abdul Salam Brigade pose for picture as they attend a training session at an undisclosed location near the al-Turkman mountains, in Syria's northern Latakia province, on April 24, 2013. AFP / MIGUEL MEDINA (Photo credit should read MIGUEL MEDINA/AFP/Getty Images)

Wapiganaji wa waasi nchini Syria

Lakini rais huyo wa Marekani pia amesisitiza kuwa ushahidi zaidi unahitajika kwa nchi hiyo kuchukua hatua kujihusisha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo tayari vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 70,000 , na hivi sasa mzozo huo unaingia katika mwaka wa tatu.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Costa rica , Obama amesema kuwa kuna ushahidi kuwa silaha za kemikali zimetumika nchini Syria, lakini ni kwamba "hatufahamu ni lini, wapi ama vipi zilitumika."

"Lakini amedokeza kuwa ushahidi wowote imara kwamba utawala wa Assad ulitumia silaha hizo utabadilisha utaratibu wa mchezo", kwa sababu silaha hizo zinaweza kuangukia katika mikono ya makundi kama kundi la wanamgambo wa Hezbollah , lililoko katika nchi jirani ya Lebanon.

Syria's President Bashar al-Assad speaks at the Opera House in Damascus in this still image taken from video January 6, 2013. REUTERS/Syrian TV via Reuters TV (SYRIA - Tags: POLITICS PROFILE TPX IMAGES OF THE DAY) NO SALES. NO ARCHIVES. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. SYRIA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SYRIA

Rais wa Syria Bashar al-Assad

"Kwa misingi ya hatua zozote za ziada ambazo tutachukua, zitakuwa katika msingi, wa kwanza ushahidi kuhusiana na kilichotokea , tena itahusiana na kile ambacho kitakuwa kwa maslahi ya watu wa Marekani na usalama wa taifa letu," ameongeza Obama.

"Kama rais wa Marekani nitafanya maamuzi hayo kwa misingi ya ushahidi sahihi na baada ya kushauriana kwa makini kwasababu iwapo tutaharakisha kufanya jambo, iwapo jutachupa kabla ya kuangalia, basi sio kwamba sisi tutaathirika lakini mara nyingi, tumeona kunatokea mambo ambayo hayakutarajiwa katika hali kama hiyo.

Ulinzi wa silaha za kemikali

Wataalamu wanasema ujumbe wa kijeshi wa kwenda kuzilinda silaha hizo za kemikali utahitaji jeshi kubwa ardhini na hiyo italeta matatizo makubwa, ambapo matokeo yatategemea uwezo wa kijasusi wa mataifa ya magharibi.

Mkuu wa zamani wa wizara ya ulinzi Leon Panetta , ambaye alijiuzulu wadhifa wake Februari mwaka huu , aliwaambia wabunge kuwa yeye pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Marekani, Jenerali Martin Dempsey, ameshauri waasi wapewe silaha lakini ushauri huo ulitenguliwa.

Nchini Syria wakati huo huo , majeshi ya serikali yameshambulia kwa mabomu maeneo ya Wasunni katika mji ulioko katika ukingoni mwa bahari ya Mediterranean wa Banias, kundi linalofanya uangalizi limesema , likionya kuhusu mauaji mapya ambapo yalisababisha watu 50 kuuwawa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Sudi Mnette

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com