Obama anaongoza lakini atakua rais ? | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.10.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Obama anaongoza lakini atakua rais ?

Mjadala wa mwisho wa TV kati ya seneta Obama na MCcain.

Seneta Obama.

Seneta Obama.

Duru ya tatu na ya mwisho ya mjadala-moto-moto kati ya wagombea wawili wa urais wa Marekani - Seneta John McCain wa Republikan na seneta Barack Obama wa Democratic party, ilipita usiku wa jana katika TV.Wingi mkubwa wa Wamarekani wamemtawaza Barack Obama kuwa ni mshindi wa mjadala huo.

Mtetezi wa chama cha Republikan John McCain,amepania sasa kutumia wiki 3 zilizosalia kabla uchaguzi hapo Novemba 4 kufanya juhudi zaidi ili kumpiku Obama,lakini upepo mkali unampiga usoni-asema Christina Bergmann katika uchambuzi wake kutoka Washington, mnaosimuliwa humu studioni na Ramadhan Ali:

Mijadala 3 ya wagombea hao wa kiti cha urais ,haikuibua mengi mapya na ya kusangaza.Yule ambae amewachunguza kwa makini watetezi hawa wawili-anafahamu sasa ni mawazo gani anayo mdemocrat Seneta Obama na yepi anayo Mrepublikan John McCain kuhusu kodi za mapato,afya na sera za nishati.

Lakini mjadala wa jumla ya saa 4 na nusu katika TV ulikuwa na madhumuni nyengine.Ulidhihirisha tofauti za kimsingi katika tabia za watetezi hawa wawili wanaoania wadhifa mkuu kabisa wa Marekani.

Kwanza seneta Barack Obama asdie na maarifa makubwa ya kisiasa,lakini anaeelewa anataka nini katika kuparamia ngazi ya kisiasa na kufikia kileleni kama Muamerika wa kwanza wa asili ya kiafrika kugombea wadhifa huo.Akiwa njiani kufikia shabaha hiyo, Obama hakufanya makosa mengi na hakukawia pia kujifunza haraka kucheza karata za kisiasa. Kwamba katika mjadala wa kwanza na John McCain ,Obama akimuunga mkono mara kwa mara aliosema,aligeuza mtindo huo wakati wa mjadala wapili.Alijitokeza kuwa mtulivu na makini na anaejiamini.hii ilitosha kumpiku hasimu yake,kwani mnamo wiki chache zilizopita,Obama alijua ameshamtupa nyuma mno mpinzani wake.

Tofauti na mpinzani wake Mrepublikan John McCain,hakumudu kuupanua zaidi uongozi aliouapata katika uchunguzi wa maoni baada ya kuteuliwa rasmi mtetezi wa chama huko St.Paul seuze kuuseleleza.

John McCain anakabiliwa na tatizo moja: anajitambulisha binafsi ni mpinzani katika chama chake kua ni mwanasiasa anaefuata njia yake mwenyewe na kwamba katika maswali mengi ana sera tofauti na zile za chama hiki cha wahafidhina.Hatahivyo, McCain ni mtetezi rasmi wa chama hicho cha Republikan.Kwahivyo, kampeni yake inatatanisha.

Seneta McCain amejaribu kulipoza moyo bawa la wahafidhina la chama cha republikan kwa kumteua makamo-wake-rais bibi Sarah Palin,mhafidhina mkubwa gavana wa Alaska.Kwa kufanya hivyo amewaudhi wapigakura wasioelemea chama chochote.wakati bibi Palin amemhusicha seneta Barack Obama na magaidi, mwenzake John MCcain anadai Obama ni mtu mwenye adabu na hershima.

Bado uchaguzi haukupita na bado seneta Barack Obama hakushinda.Na bado pia hakuna uhakika iwapo wapigakura wengi wa Marekani kweli wako tayari sasa kumchagua mtu mweusi kuwa rais wao....

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com