Obama akutana na Abbas na Netanyahu Washington | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Obama akutana na Abbas na Netanyahu Washington

Juhudi mpya za kutafuta amani baina ya Israel na Wapalestina zagubikwa na mauaji ya Waisraeli wanne huko Ukingo wa Magharibi

Rais wa Marekani, Barack Obama (katikati) waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanjahu (kushoto) na rais wa Wapalestina Mahmud Abbas

Rais wa Marekani, Barack Obama (katikati) waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanjahu (kushoto) na rais wa Wapalestina Mahmud Abbas

Rais wa Marekani Barack Obama amefanya mazungumzo na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu mjini Washington usiku wa kuamkia leo. Mkutano huo umefanyika kabla kuanza tena leo mazungumzo ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili katika kipindi cha karibu miaka miwili. Akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu yake mjini Washington rais Obama amesema Marekani haitayumbishwa katika kuhakikisha usalama wa Israel.

Juhudi mpya za amani zimegubikwa na mauaji ya Waisraeli wanne na kundi la Hamas Jumanne usiku karibu na makaazi ya Wayahudi ya Kiryat Arba, katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Kundi hilo limeapa kupinga juhudi za amani na kusema rais Abbas hana haki ya kufanya mashauriano kwa niaba ya Wapalestina.

 • Tarehe 02.09.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P2Dy
 • Tarehe 02.09.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/P2Dy
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com