Obama akataa umakamo wa rais kwa Clinton | Habari za Ulimwengu | DW | 11.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Obama akataa umakamo wa rais kwa Clinton

Barack Obama wa chama cha Demokratik amekejeli wazo la kuwa mgombea mwenza wa Hillary Clinton katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka huu.

COLUMBUS

Akizungumza katika jimbo la Mississipi hapo jana seneta huyo wa Illinois amesema wapiga kura wanapaswa kutofikiria wanaweza kuwaingiza wagombea wote wawili kwa tiketi ya chama cha DemokratikM kwa kumteuwa Clinton kugombea nafasi ya urais na kudhani kwamba yeye atakubali nafasi ya makamo wa rais.

Obama amesema inabidi watu wachaguwe kati ya wagombea hao wawili na kwamba hadi hivi sasa ameshinda katika majimbo zaidi,kura na wajumbe kuliko Clinton na anafikri atashinda uteuzi wa kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Demokratik.

Jimbo la Mississipi leo linafanya uchaguzi wa awali wa uteuzi huo wa wagombea urais nchini Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com