Obama akamilisha ziara ya ghafla Afghanistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 29.03.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Obama akamilisha ziara ya ghafla Afghanistan

Rais Barack Obama wa Marekani anaelekea nyumbani baada kufanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan hapo jana Jumapili.

default

Rais Obamana mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai

Hii ni ziara yake  ya kwanza  ya taifa hilo linalozongwa na vita tangu aingie madarakani.Akiwa mjini Kabul,Rais Obama alikutana na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai na akamsisitizia umuhimu wa uongozi bora kwa kupambana na rushwa na  ufisadi pamoja na kudumisha sheria.

Obama / Afghanistan / Bagram / USA / NO-FLASH

Rais Obama akiwahutubia wanajeshi wa Marekani katika kambi ya Bagram

Kamanda huyo  mkuu wa jeshi  la Marekani alikutana pia na vikosi  vya nchi yake katika kambi iliyokuwa karibu ya Bagram alikowahakikishia kuwa serikali itafanya kila iwezalo ili majukumu yao yafanikiwe.Rais Obama aliutilia mkazo umuhimu wa wajibu wa Marekani  wa kuendelea kupambana na wapiganaji wa Taleban pamoja na ugaidi ulio na mafungamano na kundi  la Al Qaeda.

 • Tarehe 29.03.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MgVi
 • Tarehe 29.03.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/MgVi
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com