Obama aanza ziara rasmi nchini Ujerumani na Ufaransa. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 05.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Obama aanza ziara rasmi nchini Ujerumani na Ufaransa.

rais wa Marekani Barack Obama leo Ijumaa alikutana na mwenyeji wake kansela wa Ujerumani Angela Merkel

default

Rais wa Marekani , Barack Obama, akiwa pamoja na mwenyeji wake kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Rais wa Marekani Barack Obama amekutana leo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel mwanzoni mwa ziara yake ya siku mbili katika kumbukumbu ya vita vikuu vya pili vya dunia, pamoja na nafasi mpya ya kushughulikia masuala ya kidiplomasia kati ya Marekani na Ulaya.


Rais Obama alikutana na kansela Angela Merkel mapema leo Ijumaa mjini Dresden, mahali ambapo majeshi ya washirika katika mwezi wa mwisho wa vita vikuu vya pili vya dunia waliusambaratisha mji huo na kuuwa watu wanaokadiriwa kufikia 35,000.

Baada ya mazungumzo kuhusu sera, viongozi hao wawili walikuwa na mkutano na waandishi wa habari ambapo kansela wa Ujerumani aliisifu hotuba ya rais Obama mjini Cairo na kusema kuwa itakuwa ni sehemu muhimu ya kuanzia kwa ajili ya juhudi za kuleta amani katika mashariki ya kati.

Rais Obama amesema kuwa muda umefika kuchukua hatua kuweza kusukuma mbele hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati. Pia amesema kuwa ana matumaini makubwa kuwa Marekani na inaweza kuiongoza dunia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na mporomoko wa uchumi wa dunia. Amesema rais Obama kuwa yeye pamoja na kansela Angela Merkel wamekuwa na majadiliano ya maana. Ameongeza kuwa "tunaendelea kufanyakazi kwa pamoja na kupambana na mzozo wa kiuchumi duniani ili kurejesha ukuaji na hali8 bora kwa watu wetu".


Kuhusu amani ya mashariki ya kati rais Obama amesema kuwa , tunataka kuondoa baadhi ya hali ya kutofahamiana ili tuweze kuwa na majadiliano ya ukweli, akimaanisha mazungumzo kati ya Israel na Palestina. Kwa hili tunahitaji washirika imara ameongeza.

Merkel amesema kuwa Ujerumani inapenda kuwa na taifa salama la Israel pamoja na taifa la Palestina.

Kuhusu masuala ya usalama wa dunia rais Obama alisema, Ujerumani imekuwa mshirika imara wa NATO, na kama inavyofahamika kuwa kuna changamoto kubwa nchini Afghanistan na pia Pakistan, lakini wajibu wetu wa pamoja wa kuhakikisha kuwa vituo vya magaidi ambavyo vinaleta hatari kwa watu wetu tunaendelea kupambana navyo kwa jumla.


Viongozi hao wawili walikutana kwa muda wa saa moja mwanzoni mwa ziara ya rais Obama ya siku moja nchini Ujerumani, ziara ambayo itamfikisha pia katika makambi ya zamani ya mateso ya Wanazi mjini Buchenwald, ambako zaidi ya wafungwa 56,000 waliuwawa.

Baadaye anatarajiwa kuwatembelea wanajeshi wa Marekani waliojeruhiwa katika kituo cha matibabu cha Landstuhl, na kukamilisha ziara yake katika maadhimisho ya mwaka ya 65 wa kumbukumbu ya siku majeshi ya Marekani yalipoingia Normandy nchini Ufaransa hapo kesho.


►◄
 • Tarehe 05.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I3zz
 • Tarehe 05.06.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/I3zz
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com