1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyumba za wanasiasa wa upinzani zimeshambuliwa Burundi

21 Agosti 2007

Nchini Burundi watu wasiojulikana wameshambulia kwa guruneti nyumba za wanasiasa watano wanaopinga uongozi wa nchi.

https://p.dw.com/p/CH9N
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Rais Pierre Nkurunziza wa BurundiPicha: AP

Kisa hicho kimetokea mjini Bujumbura na kuhusisha mwanasiasa mmoja wa chama tawala na naibu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani FRODEBU. Polisi wanaendelea na uchunguzi japo hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. Wakati huo huo wabunge 69 waliwasilisha barua kwa Rais Perre Nkurunziza na kutoa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Chama tawala nchini humo CNDD-FDD kinakabiliwa na mvutano wa kisiasa baada ya mwenyekiti wake maarufu Hussein Rajabu kuondolewa kwa madai ya kusababisha vurugu.

Mwandishi wetu Amida Issa anaripoti zaidi kutoka Bujumbura.