1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nouakchout. Rais wa Ujerumani ziarani Afrika.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1L

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amewasili nchini Mauritania , wakati akiendelea na ziara yake ya wiki moja katika bara la Afrika. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Ujerumani kufanya ziara katika nchi ya Kiislamu. Wakati wa ziara yake, ikiwa ni ya nne katika bara la Afrika tangu kushika wadhifa huo, Köhler analenga katika ushirikiano wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na hali bora ya biashara sawa kwa mataifa ya Afrika, misaada ya maendeleo , na tatizo la wakimbizi.