1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NOUAKCHOTT: Waafrika 50 wamefariki baharini

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79V

Muaritania na Hispania zimesema,hadi Waafrika 50 wamefariki katika Bahari ya Atlantik.Watu hao walikuwa wakisafiri kutoka Senegal kuelekea Visiwa vya Canary nchini Uhispania.Walinzi wa pwani wa Mauritania,walikuta wahamiaji wengine 96 wa Kiafrika katika boti hiyo.Kwa mujibu wa maafisa wa Mauritania na Hispania,kundi hilo liliishiwa na mafuta na wahamiaji hao walikuwa baharini kwa zaidi ya majuma mawili bila ya chakula.