Nini matarajio ya mkutano wa G-20 na wahamiaji wa kiafrika ulaya ? | Magazetini | DW | 01.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Nini matarajio ya mkutano wa G-20 na wahamiaji wa kiafrika ulaya ?

Kwanini nchi za ulaya zatumbua macho tu juu ya hatima ya wafamaji ?

Brown na Obama (London)

Brown na Obama (London)

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yametuwama juu ya mada mbali mbali tangu nchini hata nje:Matarajio ya mkutano wa kundi la mataifa 20 tajiri juu ya msukosuko wa uchumi G-20 mjini London, mpango wa Euro bilioni 50 uliochangiwa na serikali ya Ujerumani kukabiliana na msukosuko huo na hatima ya wakimbizi wa kiafrika wanaopoteza maisha yao kila kukicha baharini katika kiu chao cha kuhamia ulaya:

Gazeti la DRESDNER NEUESTE NACHRICHTEN kuhusu mkutano wa kundi la G-2o mjini London laonya:

"Pasitokee mtu kutarajia miujiza kutoka mkutano huo wa kilele wa kundi la mataifa 20 tajiri.Lakini yaweza kutazamiwa vikwazo kwa mabenki na biashara zao katika masoko ya fedha.Mtindo wa uvumi kwenye masoko ya fedha unapaswa kutoka sasa kupigwa marufuku.Hataghivyo, mfumo mpya wa mabenki utakaoibuka usiyaporome na kuyaangusha kabisa mabenki.Yafaa pia kutumai kuwa Kanzela Angela Merkel na mpango wake wastani wa kuufufua uchumi ataweza kutamba mbele ya Rais Obamya wa Marekani ambae kwa kujitwika madeni makubwa anapalilia mfumko wa bei na kukitwika mziogo wa kulipa madeni hayo kizazi kijacho.Madeni au busara-ndilo swali kuu katika mkutano wa London."

Gazeti la Schwabische Zeitung likiuchambua ule mpango wa kustawisha uchumi wa serikali ya Kanzela Merkel laandika:

"Serikali ya Ujerumani imepitisha matumizi ya Euro bilioni 50 kwa ajili hiyo na kima hicho -sehemu yake ndogo tu imeanza kutumika .Hii inatokana kwa kadri fulani na mfumo wa shirikisho wa Ujerumani.Kwanza, wilaya na majimbo kuanza matumizi ya mahitaji yao na halfu serikali yenyewe ya shirikisho.Mwishoe ,,jukumu litaangukia mabegani mwa serikali kuu kuamua kati ya kuutia jeki uchumi na klitupa jukumu la mzigo kichwani mwa kizazi kijacho."

Hautapita muda -laandika gazeti la Hannoversche Allgemeine, vigogo vya Urusi, rais Medwedew na waziri wake mkuu Putin, watatambua kwamba kutoa uhuru zaidi na kuruhusu hali ya uwazi zaidi kutaiongoza Urusi kwenye neema ya kiuchumi.Gazeti laongeza:

"Mchanganyiko wa uongozi wa kimabavu na kuzorota kwa uchumi ni hali wanaojionea wananchi na Urusi yenyewe wakati huu.Nchini Urusi kama ilivyo kwenego mfano wa China,darasa jipya la kujifunza ni hili: Udikteta haukulindi na umasikini."

Likitugeuzia mada na kugusia hatima ya mamia ya wakimbizi wa Afrika wanaokufa baharini kwa kutapia kuja ulaya-gazeti la Nordwest-Zeitung laonya:

"vifo vya wakimbizi hawa vinatokea mara nyingi bila ya kuhanikiza na mara nyingi hata havidhukuriwi.Takriba kila kukicha wanadamu hawa waliokata tamaa wanafunga safari katika mitumbwi ya kuvulia samaki kutoka Afrika wakielekea Ulaya.Msukosuko wa wakimbizi hawa katika bahari ya kati unazidi kutisha na ulaya imetumbua macho tu haijui la kufanya:Badala ya kuwaokoa, ulaya inatumia vikosi vyake vya wanamaji na zana za kisasa kabisa ili kuwazingia masikini wa mafukara wasije ulaya.Kwa njia hii matajiri wanautumbulia macho msiba na kuwa na hisia mbaya za kuchangia vifo vya wakimbizi wa marekebu hizo."

Muandishi:Ramadhan Ali

Mhariri: Josephat Charo