Nini kinaendelea Chemnitz mashariki mwa Ujerumani?
31 Agosti 2018Polisi wanaonekana kuwa hawana uwezo tena. Baadhi wanaonya, kwamba hali hiyo inatishia kutapakaa kila mahali nchini Ujerumani.
Si mara ya kwanza kwa wageni kufanyiwa mambo haya ya kukera. Lakini idadi ya waandamanaji wa mrengo mkali wa kulia, na kasi iliyotumika kuwakusanya, pamoja na kulemewa kwa polisi na kazi ya kudhibiti maandamano hayo mjini Chemnitz imewashitua wengi.
Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1990 kumekuwa na wimbi la matumizi ya nguvu dhidi ya wageni, na sio hivyo tu , lakini kwa kiasi kikubwa hali hiyo ilikuwa inatokea katika maeneo ya Ujerumani mashariki. Katika mwaka 2015 baada ya kuingia kwa maelfu ya wahamiaji matukio ya ongezeko la chuki dhidi ya wageni. Tangu wakati huo hali ya hewa imekuwa ya wasi wasi.
Kitu kilichozusha hali hiyo mjini Chemnitz kilikuwa mapambano yaliyosababisha kifo baina ya watu kutoka mataifa ya kigeni na Wajerumani, ambapo Mjerumani alichomwa kisu na kufariki. Mtu anayeshukiwa kufanya tukio hilo ni Msyria na mtu mwingine kutoka Iraq.
Kwa hiyo waandamanaji wa siasa kali za mrengo wa kulia walitumia tukio hilo la kuuwawa kwa mjerumani kuwa ndio sababu ya kufanya maandamano na kuchukua sheria mkononi mwao. Katika vidio inaonekana , jinsi gani waandamanaji walivyowashambulia wageni. Wanasema sisi ni wananchi , na wengine hata wakisema, Wajerumani, jamii, taifa", na pia walionekana wakitoa salamu za enzi wa utawala wa Hitler.
Kile kinachoonekana kutoka Chemnitz kinatisha kwasababu taifa linaonekana kutokuwa na uwezo, wageni, ama wale wanaotakiwa kuchukua hatua , kutokana na kundi la siasa kali wanavyofanya. Wanasiasa wameshitushwa. Mwenyekiti wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani Holger Stahlknecht, anaonya kwamba iwapo taifa na jamii haitaweza kuamua hivi sasa dhidi ya hali inayotokea, kuna jambo linaweza kutokea.
"Chemnitz inaweza kuonekana kesho kila mahali." Mtaalamu wa chama cha SPD wa masuala ya ndani Bukhard Lischka anzungumzia kuhusiana na hatari ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ujerumani. Na mwandishi habari Michel Friedman alisema wakati akizungumza na DW, matukio ya Chemnitz ni tone tu katika vuguvugu la chuki dhidi ya demokrasia. Limetawanya kundi hili mizizi katika jamii, kuliko tunavyofikiria.
Demokrasia nchini Ujerumani ni thabiti, lakini katika baadhi ya maeneo haikidhi masharti ipasavyo kuweza kuthibitisha hilo.
Huko nyuma mara nyingi jimbo la Saxsony limekuwa katikati ya matukio. Juergen Kasek wa chama cha Kijani katika jimbo la Saxony amekiambia kituo cha utangazaji cha DW kwamba, "tumekuwa na matatizo makubwa katika jimbo la Saxony la watu wenye siasa kali za mrengo wa kulia, kutoa hukumu ya bila kuhakikisha mambo, ubaguzi, hali ambayo imekumbatiwa na watu wengi katika jamii.
Michel Friedman anaamini kwamba jimbo la Saxony linakazi kubwa ya kufanya, kwa kuwa watu wanashambuliwa kwa kuwa tu wanaonekana tofauti.
Mwandishi: Hasselbach, Christoph / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Idd Ssessanga