Nigeria yatandikwa mabao 2-0 na Croatia | Kombe la Dunia 2018 | DW | 17.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Kombe la Dunia 2018

Nigeria yatandikwa mabao 2-0 na Croatia

Wawakilishi wengine wa Afrika Nigeria walitandikwa mabao 2-0 na Croatia, hii leo Ujerumani inakwaana na Mexico katika mechi iliyojaa msisimko kwasababu Ujerumani ndio mabingwa watetezi.

Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio ameahidi timu yake itawabana mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ujerumani, wakati timu hizo mbili zikikutana kwenye mchezo wao wa kwanza leo Jumapili.

Mexico wamewahi kuishinda Ujerumani mara moja katika majaribio 11. Walishinda 2-0 katika mechi ya kirafiki mwaka 1985, lakini Osorio anaamini wachezaji wake wanapaswa kupuuza rekodi mbaya ya timu yake dhidi ya mabingwa wa dunia mara nne.

Katika mechi za jana Jumamosi Ufaransa iliifunga Australia mabao 2-1, Argentina ilitoka sare ya bao 1-1 na Iceland, Denmark iliifunga Peru bao 1-0 na wawakilishi wengine wa Afrika Nigeria walitandikwa mabao 2-0 na Croatia.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni kati ya Costa Rica na Serbia na Brazil wanavaana na Uswisi. 

 

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com