Nigeria yafungwa na Ugiriki na kukalia kuti kavu | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Nigeria yafungwa na Ugiriki na kukalia kuti kavu

Nigeria imejiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu kwa raundi ya pili ya michuano ya fainali za kombe la dunia baada ya kufungwa mabao 2-1 na Ugiriki katika mechi za kundi B.

default

Beki wa Nigeria Sani Kaita akitoka nje baada ya akupewa kadi nyekundu kwa kosa la kizembe

Kwa kipigo hicho cha sasa Nigeria inalazimika kuigunga Korea Kusini mwa mabao mawili na wakati huo huo ikiombea Argentina iifunge Ugiriki bila ya wavu wake kutikiswa.

Nigeria ilikuwa ya kwanza kufunga kwa bao la Kalu Kaita katika dakika ya 16, lakini Ugiriki walisawazisha bao hilo kupitia kwa Dimitris Salpingidis katika dakika ya 44, kabla ya Vassilis Torosidis kupachika la pili katika dakika ya 71.Kutolewa kwa beki wa Nigeria Sani Kaita kwa kosa la kizembe kulichangia Nigeria kushindwa mchezo huo.

Mapema Argentina ilikuwa nchi ya kwanza kufuzu kwa raundi ya pili baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 4-1.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

 • Tarehe 17.06.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NtwW
 • Tarehe 17.06.2010
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NtwW

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com