Nigeria: Wakulima wawili wauwawa na Boko Haram | Matukio ya Afrika | DW | 27.11.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Nigeria: Wakulima wawili wauwawa na Boko Haram

Wapiganaji wa jihadi wamewauwa wakulima wanne karibu na mji wa kaskazini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguri. Wiki iliyopita, wapiganaji hao wa jihadi waliwauwa wakulima tisa na kuwateka wengine 12.

Wapiganaji wa jihadi wamewauwa wakulima wanne karibu na mji wa kaskazini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguri, ikiwa  ni  umwagikaji wa damu wa hivi karibuni katika jimbo hilo lenye matatizo, watu walioshuhudia pamoja na kiongozi wa wanamgambo wa  eneo hilo wamesema.

Wapigaji darzeni kadhaa wanaoaminika kuwa watiifu kwa kundi la Boko Haram linaloongozwa na Abubakar Shekau walishambulia  kundi la wakulima waliokuwa wakifanyakazi zao shambani karibu na Jiddari-Polo jana, ameeleza mkulima ambaye amenusurika katika shambulio  hilo.

Boko  Haram  wameongeza  mashambulio  yao  dhidi  ya wakulima  na  wakataji  mbao  katika  miaka  ya  hivi karibuni, wakiwashutumu kwa  kutoa  taarifa  juu  ya  kundi hilo  kwa  jeshi  la  Nigeria.

Wiki iliyopita, wapiganaji  hao  wa  jihadi  waliwauwa wakulima  tisa  na  kuwateka  wengine  12 katika shambulio  katika  kijiji  cha  Mammanti karibu  na Maiduguri.