1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiNigeria

Nigeria kuendelea na mageuzi ya kiuchumi

12 Juni 2024

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu amesema serikali yake itaendelea kufanya mageuzi ya kiuchumi nchini humo licha ya hali ngumu inayozidi na kusababisha ghadhabu za umma.

https://p.dw.com/p/4gxG1
Sarafu ya Naira ya nchini Nigeria
Sarafu ya Naira ya nchini NigeriaPicha: Ubale Musa/DW

Tinubu ameahidi kuwasilisha mswada wa serikali bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kuweka kiwango cha chini cha mshahara nchini Nigeria.

Tinubu ambaye aliingia madarakani mwaka mmoja uliopita, aliondoa ruzuku ya mafuta iliyoifanya bei ya bidhaa hiyo kushuka kwa njia ambayo si halisi na kuishusha thamani ya sarafu ya nchi hiyo.

Hatua hiyo ilipelekea mfumko wa bei kupanda na kufikia asilimia 33.69 mnamo mwezi Aprili, hicho kikiwa kiwango chake cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha karibu miongo mitatu.

Tinubu amesema kuondoa ruzuku ni jambo ambalo limeyafanya maisha kuwa magumu ila ni msingi thabiti wa ukuaji wa uchumi.