NICOSIA.Watu kumi na wawili waokolewa na kikosi cha wanamaji cha Ujerumani
24 Oktoba 2006Matangazo
Kikosi cha jeshi la wanamaji cha Ujerumani kimewaokowa mabaharia 12 wa meli ya Syria iliyoshika moto katika eneo la mashariki la bahari ya Mediterranean.
Jeshi la Ujerumani linalotekeleza mpango wa amani wa umoja wa mataifa katika pwani ya Lebanon liliwapeleka kwa helikopta mabaharia wawili katika hospitali ya kisiwa cha Cyprus na kuwaokowa mabaharia kumi 10 waliosalia.