Ni miaka 50 tangu kujengwa ukuta wa Berlin | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.08.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ni miaka 50 tangu kujengwa ukuta wa Berlin

Ujerumani leo inaadhimisha miaka 50 tangu kujengwa ukuta wa Berlin. Maadhimisho yamefanywa Berlin, kwa kufunguliwa makumbusho ya wale waliopoteza maisha yao, wakati walipokuwa wakijaribu kuuvuka ukuta huo

default

Ujenzi wa ukuta wa Berlin ulianza Agosti 13, 1961

Leo wajerumani wanawakumbuka wahanga wa kuta la Berlin lililojengwa miaka 50 iliyopita. Kwenye hafla iliofanyika katika mji mkuu Berlin, watu walinyamaza kimya kwa muda wa dakika moja ili kuwakumbuka wahanga hao.

Mauerbau Gedanktag Jahrestag Mauer

Kuta la Berlin lilianza kujengwa siku kama ya leo miaka 50 iliyopita, na viongozi wa sehemu iliyokuwa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani -yaani Ujerumani ya Mashariki, kwa lengo la kuufunga mpaka kati ya mji wa Berlin ya Mashariki na ya Magharibi.

Ujenzi wa Kuta hilo uliashiria hatua ya kuigawanya Ujerumani wakati huo, hadi tarehe 9 mwezi Novemba mwaka 1989 ambapo kuta hilo liliondolewa.

Mauerbau Gedanktag Jahrestag Mauer

Rais Christian Wulff, mkewe Bettina, Kansela Angela Merkel ni miongoni mwa waliokuwepo katika kumbukumbu za leo

Jumla ya Watu 136 walikufa katika nyakati mbalimbali walipojaribu kuvuka mpaka kutoka Berlin ya Mashariki ili kukimbilia Berlin ya Magharibi.

Rais wa Ujerumani Christian Wulff atatoa hotuba kwenye hafla hiyo mjini Berlin. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Meya wa jiji la Berlin, Klaus Wowereit, pia wamekuwapo kwenye hafla hiyo.

Mwandishi Maryam Abdalla/dpa/ afp/ epd
Mhariri:Mtullya Abdu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com