1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ngome ya Mugabe yatikisika

27 Agosti 2008

Nguzo anayoegemea Rais Mugabe wa zimbabwe imeanza kutikisika.

https://p.dw.com/p/F5wQ
R.MugabePicha: AP

Ngome ya utawala wa Mugabe imeanza kutikisika.

Miezi 5 tangu uchaguzi wa mizengwe,bunge limeanza shughuli zake.Licha ya wasi wasi mkubwa ,hata wabunge wa chama cha upinzani cha MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai,walikalia viti vyao Bungeni.Hatahivyo,hawakuchelea kuonesha hasira zao kwa Rais Mugabe .kwani,katika bunge la zimbabwe ,upinzani ndio wenye viti vingi zaidi.Kwahivyo,ngome ya utawala wa Mugabe imeanza kutikisika-kwa muujibu anavyochambua Ute Schaefer-mkuu wa Idhaa za afrika na Mashariki ya kati wa DW:

Kila kitu kikienda kama desturi:rais Mugabe akipakiwa ndani ya motokaa yake ya kifahari ya Rolls- royce, ametandikiwa busati jekundu akiingia bungeni kulifungua Bunge ambalo lilikuwa mhuri wa kuidhinisha tu yale aliyoamua.Kwa njia hii,rais Mugabe akitarajia kujionea sherehe za aina ile ile aliiozowea za ufunguzi wa bunge jipya pamoja na ushirikiano uile ule alioupata. hotuba yake ya dakika 30 ilioonekana katika Tv ilikatizwa mara kwa mara na vilio vya kuichafua.Wabunge wa chama cha upinzani cha MDC waligoma kusimama wima alipowasili Bungeni na wakaifuja hotuba yake.

Kwa mara nyengine,Upinzani ulioonesha ujabari wake.Licha ya mkomoto unaokumbana nao na licha ya kuandamwa mfululizuo na hatua ya Mugabe ya kuzuwia kile ambacho hataki kiwe - matokeo ya uchaguzi wa Machi kugeuka ukweli halisi wa kisiasa na kuupa Upinzani haki yake.

Katika uchaguzi wa Bunge ,upinzani ulishinda.ulijipatia viti 110 Bungeni-bunge lenye viti jumla 210.huo si wingi mkubwa hivyo,lakini ulitosha kuleta vishindo vya kisiasa nchini.

Chama-tawala cha ZANUpf cha rais Mugabe kiliondokea na viti 99 na hivyo kwa mara ya kwanza tangu uhuru 1980,hakina wingi Bungeni.

Kufuatia ushindi wao wa kwanza wa sehemu tu ya uchaguzi,Upinzani ulikwisha bainisha kuvinjari kwake pale mwanasiasa wake Lovemore Moyo, wa chama cha MDC aliposhinda uchaguzi wa spika, ikibainika alipata pia baadhi ya kura za wajumbe wa chama-tawala.

Hili ni tokeo muhimu,kwani labainisha ngome ya Mugabe, imeanza kutetereka na kuyumba yumba.

Imeanza kuyumbayumba kwa kuwa msingi wake anaoegemea, umeanza kumuachamkono.Hakuna anaefaidika na kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe kuliko sababishwa na Mugabe.Si wanabiashara wala wanajeshi wsaliopo nyuma ya Mugabe, wanaonufaika na hali hiyo.......

Upinzani lkwahivyo,umevuna mafanikio fulani,lakini haukupiga bado hatua ya kuweza kubadili kimsingi nguvu za madaraka nchini Zimbabwe.