1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neymar ataka kuendelea kubakia PSG

25 Mei 2022

Mshambuliaji wa klabu ya Ufaransa Paris Saint Germain, PSG, Neymar amesema angependa kuendelea kubakia katika timu hiyo.

https://p.dw.com/p/4BrXA
Fußball Frankreich Neymar PSG
Picha: Thibault Camus/AP/picture alliance

Licha ya kushindwa kufikia thamani yake ya rekodi ya dunia ya euro milioni 222 kimchezo, hasa wakati ambapo kuna tetesi kwamba klabu hiyo bingwa ya Ufaransa iko tayari kumruhusu aondoke. Soma Neymar akaribia kujiunga na PSG

Neymar mwenye umri wa miaka 30 raia wa Brazil alitia saini kurefusha mkataba wake mwaka jana hadi mwaka 2025.

Hata hivyo, umekuwa msimu mbaya tena kwake kutokana na jeraha ambalo linaibua maswali juu ya siku zijazo katika klubu ya PSG.

soma Messi, Neymar, Mbappe hawakufua dafu

Gazeti la michezo la L'Equipe limedai kwamba PSG haitopinga Neymar kuondoka.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alipachika wavuni bao lake la 100 kwa PSG tangu alipojiunga na klabu hiyo 2017, baada ya kuilaza Metz 5-0  Jumamosi iliyopita. soma Neymar afunga hat-trick kuizamisha Baseksehir

Bado nipo

Weltspiegel | PSG verliert Halbfinale der CL | Neymar
Picha: Phil Noble/REUTERS

Neymar amesema hajasikia fununu za yeye kuondoka PSG.

"Sijasikia kitu kama hicho, lakini kwa upande wangu ukweli ni kwamba nataka kubakia"  aliambia tovuti ya Oh My Goal.

PSG baada ya kumshawishi nyota mshambuliaji Kylian Mbappe kusaini mkataba mpya na kuipuuza Real Madrid, wanalenga kujenga kikosi madhubuti wakiwa na matumaini ya kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya, Champions.

Kuondoka kwa mkurugenzi wa michezo kutoka Brazil, Leonardo na nafasi yake kuchukuliwa na mreno Luis Campos kumeonekana kuwa jambo ambalo limeathiri pakubwa nafasi ya Neymar PSG.

 

//AFP