1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:UN yataka jeshi lake kupelekwa Somalia

21 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXD

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka katibu mkuu wa umoja huo Ban Ki-Moon kuanza utaratibu wa kupeleka kikosi cha umoja huo cha kulinda amani nchini Somalia.

Baraza hilo pia lilipitisha azimio la kuongeza kwa miezi mingine sita zaidi kuwepo kwa kikosi cha umoja wa afrika nchini humo na kuyataka mataifa ya afrika kuchangia askari katika kikosi hicho.

Umoja wa Mataifa uliridhia Umoja wa Afrika kupeleka kikosi cha askari elfu nane wa kulinda amani nchini Somalia, baada ya majeshi ya Ethiopea kuyasaidia yale ya serikali ya mpito kuwafurusha wanamgambo wa muungano wa mahakama za kiislam.Lakini mpaka sasa ni Uganda pekee ndiyo iliyopeleka askari 1,800.