1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Rais Bush aahidi kushirikiana na Umoja wa Mataifa

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZz

Rais wa Marekani George W Bush na katibu mkuu mpya wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wameahidi kushirikiana ili kujaribu kupata amani katika maeneo yanayokumbwa na vita na ghasia ulimwenguni.Kulingana na Rais Bush Marekani inataka kushirikiana na Umoja wa mataifa ili kufikia amani kwa kudumisha uhuru.Bwana Ban Ki-Moon kwa upande wake anasema kuwa Marekani na Umoja wa Mataifa wana malengo sawa.

Hata hivyo Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anasisitiza kuwa uhusiani kati ya Umoja wa Mataifa na Marekani haupaswi kudhalilisha mataifa mengine hususan yanayoendelea.

Bwana Ban Ki-Moon aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto kubwa kwani hakuna nchi inayoweza kutafuta suluhu kivyake bila ushirikiano.

Kiongozi huyo aliyasema hayo katika ziara yake ya kwanza mjini Washington tangu kuchukua wadhifa huo mwanzo wa mwaka huu.