1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.katibu mkuu ashutumu mauaji.

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBLC

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameshutumu vikali mauaji ya wanajeshi 10 wa jeshi la umoja wa Afrika la kulinda amani katika jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Wanajeshi wengine wanane walijeruhiwa na zaidi ya 40 hawajulikani waliko baada ya kambi yao ya Haskanity kuvamiawa na watu wenye silaha.

Hilo lilikuwa shambulio baya kabisa kuwahi kutokea dhidi ya wanajeshi hao 7,000 wa jeshi la umoja wa Afrika tangu pale lilipowekwa huko miaka mitatu iliyopita. Shambulio hilo linakuja kiasi cha wiki kadha kabla ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kufanyika mjini Tripoli katika juhudi za kupanua makubaliano ya amani ya Darfur yaliyotiwa saini May mwaka jana.