NEW YORK:Kansela Angela Merkel kuhutubia umoja wa mataifa kesho | Habari za Ulimwengu | DW | 24.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Kansela Angela Merkel kuhutubia umoja wa mataifa kesho

Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 150 wanakutana mjini New York kujadili mbinu za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Mkutano huo wa kimatiafa umedhaminiwa na umoja wa mataifa unatarajiwa kupanga mikakati ya mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa utakao fanyika nchini Indonesia mwezi Desemba.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon ameitolea mwito jamii ya kimataifa kuongeza jitihada za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ujerumani inawakilishwa na kansela Angela Merkel ambae anaondoka leo hii kwenda mjini New York.

Kansela Merkel kesho atalihutubia baraza kuu la umoja wamatiafa ambako anatarajiwa kuwasilisha madai ya Ujerumani kuhusu kumiliki kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kansela Angela Merkel wa Ujerumani kuhutubia mbele la baraza kuu la umoja wa mataifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com