NEW-YORK:Ban Ki-moon ayataka makundi hasimu darfur kuvumiliana | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW-YORK:Ban Ki-moon ayataka makundi hasimu darfur kuvumiliana

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameyataka makundi yote yanayohusika katika mzozo wa jimbo la Darfur kuvumiliana na kuweka amani katika eneo hilo. Ban Ki Moon anatarajiwa kufanya ziara Darfur wiki ijayo pamoja na Chad na Libya.

Lengo kuu la ziara yake nchini Sudan ni kuweka misingi ya amani ya kudumu kwenye jimbo la mgogoro la Darfur.

Katibu mkuu huyo amewaambia waandishi wa habari kwamba pamoja na kuwa wanajeshi wa kuweka amani watakwenda Darfur,usalama hauwezi kupatikana bila kuweko ushirikiano kutoka serikali ya Sudan na kwa hivyo ataibinya serikali hiyo kuunga mkono kikamilifu juhudi za kuleta amani Darfur.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com