New York. Wolfowitz abanwa zaidi ajiuzulu. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Wolfowitz abanwa zaidi ajiuzulu.

Mbinyo dhidi ya mkurugenzi mkuu wa benki ya dunia Paul Wolfowitz unaongezeka kufuatia mkutano wa wakurugenzi wa bodi ya taasisi hiyo.

Wolfowitz anakumbana na miito kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo ili ajiuzulu kuhusiana na alivyoshughulikia kupandishwa cheo kwa mpenzi wake wa kike ambaye ni mwajiriwa wa benki hiyo.

Katika mazungumzo yaliyochukua muda mrefu hadi usiku wa jana Alhamis , bodi hiyo yenye wajumbe kutoka mataifa 24 imesema kuwa imekubaliana kuchukuliwa hatua za haraka katika kupambana na uwezekano wa kulinda maslahi.

Wolfowitz ameombwa kufanya mabadiliko katika utawala lakini amekataa kujiuzulu, kitu ambacho wapinzani wake wanakidai.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com