NEW YORK : Wanawake wa Kiarabu wakabiliwa na ubaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Wanawake wa Kiarabu wakabiliwa na ubaguzi

Repoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba wanawake katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa ambao unakwamisha uchumi na ustawi wa jamii wa eneo hilo.

Repoti hiyo iliotayarishwa na wataalamu wa Kiarabu na wanataaluma inasema wanawake wa Kiarabu lazima wapatiwe nafasi ya elimu,huduma za afya na fursa za kiuchumi.Repoti inasema nusu ya wanawake wa Kiarabu hawawezi kusoma au kuandika.Mahudhurio katika shule za sekondari miongoni mwa wasichana ni chini ya asilimia 80 katika nchi zote za Kiarabu isipokuwa nne tu.

Ukosefu wa ajira kwa wanawake uko juu mara mbili hadi tano kuliko ule wa wanaume na wanawake hufanya asilimia 10 tu ya wabunge wa Kiarabu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com