1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vikosi vya amani vimeongezewa muda kubakia Kongo

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRj

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepiga kura kurefusha kwa miezi miwili mingine muda wa vikosi vya amani kubakia nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Hatua hiyo itampa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alieizuru Kongo mwezi uliopita,nafasi ya kutoa ripoti kuhusu uwezekano wa kurekebisha vikosi vya Umoja wa Mataifa.Tume hiyo ikiwa na wanajeshi 18,000 ni ujumbe mkubwa kabisa wa Umoja wa Mataifa kote duniani.Shirika la misaada la OXFAM lakini limeonya,hatua ya kupunguza vikosi hivyo huenda ikaathiri yale maendeleo yaliopatikana Kongo tangu nchi hiyo mwaka jana kuwa na uchaguzi wake wa mwanzo baada ya miaka 40.Wakati huo huo, Ban ameonya dhidi ya vikwazo vya kulenga biashara haramu ya madini.Amesema,hatua hiyo huenda ikasababisha ghasia za kijamii na kuleta madhara. Hapo awali,wataalamu wa Umoja wa Mataifa walitoa wito wa kukomosha uporaji wa dhahabu na almasi. Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kadhaa,wananchi wa Kongo wana matumaini ya kuwa na amani,kufuatia uchaguzi wa Oktoba mwaka 2006.