New York. Umoja wa mataifa washutumu mauaji ya waandishi habari. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Umoja wa mataifa washutumu mauaji ya waandishi habari.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeshutumu mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari katika maeneo ya vita.

Mwaka huu waandishi habari 55 wamepoteza maisha yao wakati wakifanyakazi, 32 kati yao nchini Iraq.

Umoja wa mataifa umezitaka serikali pamoja na pande zote zinazohusika katika maeneo ya mizozo, kufanya kila linalowezekana kuzuwia uhalifu dhidi ya waandishi wa habari, kuchunguza uhalifu wa aina yoyote uliotokea na kuwawapeleka wale wote wanaohusika mbele ya sheria.

Nchi ya pili ambayo inahatari kubwa kwa waandishi wa habari ni Afghanistan, ikifuatiwa na Phillipines, kwa mujibu wa kamati inayowalinda waandishi wa habari yenye makao yake makuu mjini New York.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com