NEW YORK : Sudan yumkini kuridhia kikosi cha pamoja Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Sudan yumkini kuridhia kikosi cha pamoja Dafur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema hapo jana kwamba anategemea Sudan kuridhia hivi karibuni kikosi cha pamoja cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kusaidia kukomesha umwagaji damu kwenye jimbo la Dafur.

Annan amesema amepokea repoti za kutia moyo kutoka kwa mwakilishi wake huko Khartoum Ahmedou Ould- Abdallah ambaye amezungumza na Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan.

Lakini ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika hotuba ya kuaga kwamba halichukulii jambo hilo kama la kawaida tu baada ya kuwepo kwa hali ya kukatisha tamaa mara kadhaa kwa hiyo amesema Umoja wa Mataifa kwanza unahitaji kuona waraka utakaoletwa na Ould-Abdallah.

Kwa mujibu wa Annan repoti alizopokea zimemshajiisha na kumfanya afikirie kwamba yumkini leo wakapata ruhusa ya Rais Bashir ya kuwekwa kwa kikosi hicho.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com