1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York: Mhamiaji wa Kipakistan apewa kifungo cha miaka 30 gerezani Marekani kwa kupanga kukiripua kituo cha gari moshi.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHj

Mahakama ya Marekani imemhukumu mhamiaji wa Kipakistani kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kufanya njama ya kuripua bomu katika kituo cha treni inayopita chini ya ardhi mjini New York. Siraji Shahawar, mwenye umri wa miaka 24, alipatikana na hatia mwezi Mei mwaka jana kufanya njama ya kukiripuwa kituo cha gari moshi ambacho kiko karibu na eneo lenye maduka mengi. Siraj Shahawar alikamatwa Agosti mwaka 2004, na alipatikana na hatia , kwa sehemu, kutokana na ushahidi wa shushushu wa polisi. Mawakili wa utetezi walihoji kwamba shushushu huyo alitumia vibaya madaraka yake ya upelelezi ili kumnasa Siraj.