NEW YORK: Marekani yashutumu Umoja wa Mataifa kwa msaada wa kifedha kwa Korea Kaskazini. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Marekani yashutumu Umoja wa Mataifa kwa msaada wa kifedha kwa Korea Kaskazini.

Marekani imelishutumu Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa madai kwamba huenda mamilioni ya fedha za msaada zilitolewa kwa serikali ya Korea Kaskazini ya Kim Jong Il.

Naibu balozi wa Marekani wa Umoja wa Mataifa, Mark Wallace, amelishutumu shirika hilo kwa kukiuka kwa muda mrefu kanuni za Umoja huo liliporuhusu fedha kupelekwa katika taifa hilo la Kikomunisti.

Mark Wallace amesema kuna wasiwasi huenda fedha hizo zimetumika kugharamia mradi wa silaha za kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Wakuu wa Umoja wa Mataifa wamesema watafanya uchunguzi kamili kuhusu suala hilo na kwamba watumishi wa Umoja huo walioko Korea Kaskazini watakuwa wakilipwa mishahara yao kwa sarafu ya taifa hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com