1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Marekani na Ufaransa zataka vikwazo dhidi ya Iran

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByn

Marekani na Ufaransa zimesema zinaiunga mkono hatua ya kuiwekea Iran vikwazo vipya kwa kuendelea kurutubisha madini ya uranium kinyume na matakwa ya Umoja wa Mataifa.

Nchi hizo zimetangaza hayo baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia nishati ya nyuklia, IAEA, kutangaza Iran imepuuza tarehe ya mwisho iliyowekewa isimamishe urutubishaji wa madini ya uranium.

Mkuu wa shirika hilo, Mohammed el-Baradei amesema anaamini Iran inahitaji kati ya miaka mitatu hadi miaka minane ifikie hatua ya kutengeneza silaha za kinyuklia.

Mataifa ya magharibi yamekuwa yakishuku Iran kwamba imepania kuutumia mradi wake huo kutengeza silaha za kinyuklia, lakini taifa hilo limekuwa likikanusha madai hayo.