New York: Maandamano makubwa katika miji ya Marekani kupinga vita vya Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York: Maandamano makubwa katika miji ya Marekani kupinga vita vya Iraq

Maelfu kwa maelfu ya watu waliandamana katika zaidi ya miji 12 ya Marekani, kutoka New York hadi San Francisco, wakitaka vita vya Iraq vikomeshwe kwa haraka. Pia waanadmanaji hao waliwataka wabunge wa Marekani kuizuwia serekali kugharamia vita hivyo. Walipinga uwezekano wa kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya Iran. Muungano wa jumuiya kadhaa za kisiasa, kijamii na kidini uliandaa maandamano hayo yaliosadifu kutimia miaka mitano tangu bunge la Marekani lilipoamuru viendeshwe vita dhidi ya Iraq. Mabarabara yalijaa maelfu kwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga vita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com