NEW YORK: Gambari kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 03.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Gambari kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Irak

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon amemteua mwanadiplomasia wa Kinigeria kama mjumbe wake maalum,kuhusika na misaada ya umoja huo kuijenga upya Irak.Ibrahim Gambari,ataratibu misaada ya Umoja wa Mataifa kwa Irak kuambatana na mradi wa ushirikiano uliokubaliwa mwezi wa Julai mwaka 2006.Umoja wa Mataifa,katika kipindi cha miaka mitano ijayo,kwa idhini ya Benki Kuu ya Dunia,unatazamia kusaidia kazi za kuijenga upya Irak.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com