1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la usalama lataka majeshi ya umoja wa mataifa yapelekwe Somalia

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5T

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka katibu mkuu wa umoja huo, Ban Ki Moon, aanzishe mpango wa kuwapeleka wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kwenda Somalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1995.

Mapigano baina ya wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somali wakisaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia dhidi wanamgambo wa kiislamu yamesababisha vifo vya Wasomali zaidi ya 1000.

Kwa mujibu wa mashirika ya kutoa misaada ya kiutu Wasomali takriban laki nne walilazimika kuyahama makaazi yao.

Katika taarifa yake, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka katibu mkuu, Ban Ki Monn, atoe ripoti kufikia katikati ya mwezi ujao kuhusu mpango utakaojadili uwezekano wa kutuma kikosi cha kulinda amani nchini Somalia.

Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa, Emyr Jones Parry, aliyemaliza jana uenyekiti wa baraza la usalama, alisema kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Somali hakitarajiwi kutumwa hivi karibuni.