1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Baraza la Usalama laidhinisha kutuma vikosi Darfur

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy9

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha mpango wa kupeleka Darfur zaidi ya wanajeshi na polisi 23,000 kuwalinda raia katika eneo hilo lililokumbwa na vita magharibi mwa Sudan.Pendekezo la kupeleka kikosi kinachojumuisha majeshi ya Umoja wa Afrika na ya Umoja wa Mataifa tayari limewasilishwa kwa balozi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa,ili lipate idhini ya serikali ya Khartoum.Baraza la Usalama limeyataka makundi yote husika yaunge mkono mchakato huo wa kisiasa na kukomesha mashambulizi dhidi ya raia na wanajeshi wa kulinda amani na kuruhusu misaada ya kiutu.