NEW YORK: Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa majeshi yake nchini Ivory Coast. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa majeshi yake nchini Ivory Coast.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuongeza muda kufikia tarehe thelathini mwezi Juni kwa vikosi vyake na pia vya Ufaransa vinavyolinda amani nchini Ivory Coast.

Wanajeshi zaidi ya elfu nane wa Umoja wa Mataifa na wengine elfu nne wa Ufaransa wamekuwa nchini humo tangu mwezi Novemba mwaka uliopita kuhakikisha kutekelezwa mwafaka wa amani kati ya majeshi ya serikali ya Rais Laurent Gbagbo na vikosi vya waasi.

Baraza hilo limewataka wanajeshi hao kusaidia kuyavunja makundi ya waasi na pia kusaidia katika maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanywa tarehe thelathini na moja mwezi Oktoba mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com