1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Baraza kuu la umoja wa mataifa kuidhinisha usitishaji wa adhabu ya kifo.

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CI1g

Jopo la baraza kuu la umoja wa mataifa limeidhinisha azimio linalotoa wito wa kusitishwa kwa adhabu ya kifo. Kura hiyo iliyoidhinisha suala hilo ambalo linaleta mvutano ni 99 zilizosema ndio na 52 zilizokataa na 33 hawakupiga kura.Marekani imejiunga na mataifa mengi yanayoendelea kupiga kura ya hapana. Baraza kuu la umoja wa mataifa lenye wajumbe 192 linatarajiwa kuidhinisha uamuzi huo, huenda mwezi ujao, kwa mujibu wa wanadiplomasia.