NEW YORK: Ban Ki-Moon kuanza kazi leo | Habari za Ulimwengu | DW | 02.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ban Ki-Moon kuanza kazi leo

Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon anatarajiwa kuanza kazi hii leo mjini New York Marekani. Ban atazungumza na wafanyakazi wa umoja wa mataifa wanaosubiri kwa hamu kubwa kuhusu ajenda yake na nani watakaoteuliwa kuchukua nyadhifa muhimu katika umoja huo.

Tangu alipoidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Ban Ki-Moon hajasema lolote kuhusu mipango yake lakini ameyatembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa mara moja akiwa ameandamana na marafiki zake kutoka Korea.

Mwishoni mwa juma lililopita mwandishi wa habari mwanamke kutoka Haiti, Michele Montas, aliteuliwa kuwa msemaji mkuu wa katibu mkuu, Ban Ki-Moon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com