NEW YORK: Ban Ki Moon alaani shambulio la bomu dhidi ya treni nchini India | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ban Ki Moon alaani shambulio la bomu dhidi ya treni nchini India

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani vikali shambulio la bomu dhidi ya treni ya abiria nchini India.

Watu takriban 66 waliuwawa katika shambulio hilo wakati treni hiyo ilipokuwa njiani kwenda Pakistan ikitokea mjini New Delhi nchini India.

Ban Ki Moon amesema ametiwa moyo na hatua ya viongozi wa India na Pakistan kuapa kutoruhusu shambulio hilo kuzikwamisha juhudi za kutafuta amani.

Katika taarifa yake katibu mkuu huyo amesema kitendo hicho kiovu hakiwezi kukubalika kwa vyovyote vile na akataka waliohusika katika shambulio hilo wachukuliwe hatua kisheria.

Wakati haya yakiarifiwa, polisi nchini India wamemkamata mshukiwa wa kwanza anayetuhumiwa kuhusika na shambulio dhidi ya treni hiyo ya abiria.

Polisi pia wanamtafuta mwanamume mwingine anayeaminiwa alihusika katika shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com