NEW YORK: Ban Ki Moon aitaka Sudan iheshimu mkataba wa amani | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ban Ki Moon aitaka Sudan iheshimu mkataba wa amani

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ameitolea mwito serikali ya Sudan na waasi wa zamani wa eneo la kusini wauheshimu mkataba wa amani uliovimaliza vita vya miongo kadhaa. Aidha katibu mkuu huyo ameonya dhidi ya mjadala wa kujihami.

Kundi la waasi la Sudanese Liberation Movement, SPLM, liliwaondoa mawaziri wake katika srikali ya mseto mwezi uliopita, likiilaumu serikali kwa kushindwa kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa mnamo mwaka wa 2005 ambayo yalivimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sambamba na hayo, baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesema ni muhimu kuendelea na mpango wa kupeleka kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia licha ya Ban Ki Moon kusema wazo hilo haliwezi kutekelezwa kwa wakati huu.

Mapema mwezi huu Ban Ki Moon alisema usalama nchini Somalia ni mbaya mno kiasi kwamba haiwezekani kutuma timu ya maafisa kutathimini hali ilivyo nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com