NEW YORK . Ban aitaka Marekani kuifunga Guantanamo | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK . Ban aitaka Marekani kuifunga Guantanamo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka Marekani kufunga kambi yake ya mahabusu ya kijeshi huko Guantanamo nchini Cuba.

Ban alikuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya kuwasili kwa mahabusu wa kwanza katika kambi hiyo ya wafungwa baada ya kutekwa wakati wa uvamizi uliongozwa na Marekani nchini Afghanistan.Mamia ya watuhumiwa wa ugaidi wanashikiliwa kwenye kambi hiyo takriban wote bila ya kuzingatia taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahkamani au kupatiwa ushauri wa kisheria.

Maandamano pia yamefanyika duniani kote kuitaka Marekani kufunga kambi hiyo ya Guantanamo.

Miongoni mwa waandamanaji ni kundi lililoandamana karibu na uzio ambao unalitenganisha gereza hilo la Marekani na Cuba nzima.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com