1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Annan ataka hatua kwa suala la Dafur

12 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjw

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekitaka chombo cha dunia cha kulinda haki za binaadamu kutuma ujumbe wa wazi kwamba jinamizi la umwagaji damu huko Dafur lazima likomeshwe.

Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa linakutana mjini Geneva katika kikao cha dharura kujadili hali ya jimbo hilo lenye vurugu la Dafur.Katika kujadili iwapo kutuma ujumbe maalum wa uchunguzi huko Dafur maafisa wanasema zaidi ya watu 200,000 wameuwawa tokea kwama 2003.

Kamishna wa Haki za Buinaadmu wa Umoja wa Mataifa Loise Arbour amesema kwamba raia wanaendelea kushambuliwa kwa makusudi na kutendewa vitendo vya ukatili.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kwamba wakimbizi 20,000 wa Sudan wataanza kurudi nyumbani wiki hii huko kusini mwa Sudan kutoka Ethiopia na Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati operesheni yake ya kuwarudisha nyumbani wakimbizi ikizidi kutanuka.