NEW DELHI: Waasi wavamia vikosi vya usalama nchini India | Habari za Ulimwengu | DW | 24.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI: Waasi wavamia vikosi vya usalama nchini India

Si chini ya wanajeshi 15 wameuawa baada ya kuvamiwa katika jimbo la Manipur,kaskazini-mashariki mwa India.Maafisa wanawashuku waasi wanaogombea kujitenga katika eneo hilo.Wamesema, kikosi maalum kinachopambana na uasi na kilichokuwa kikipiga doria,kilifyatuliwa risasi na wanamgambo katika wilaya ya Bishenpur inayopakana na Burma.Ripoti zinasema,zaidi ya watu 10,000 wameuawa katika uasi wa eneo hilo katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com